Tuesday, July 10, 2012

WENGINE haoooooooo W




MPAMBANO WA WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA LEO

Saturday, July 7, 2012
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Arimeru Mashariki (Chadema)  Joshua Nasari kabla ya mechi ya wabunge mashabiki wa Yanga na Simba, kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi. Yanga walilala kwa mabao 3-2 baada ya kupigiana mikwaju ya penati kufuatia timu hizo kushindwa kufungana katika dakika tisini za mchezo huo.
 Kikosi cha wabunge wa Yanga
 Kikosi cha Wabunge wa Simba
 Benchi la Yanga
 Wachezaji wa akiba wa timu ya wabunge mashabiki wa Yanga
 Joshua Nassari wa timu ya wabunge mashabiki wa Simba (kushoto) akipambana na Michael Kadebe wa Yanga
 Zitto Kabwe (kushoto) wa Simba akichuana na beki wa timu ya Wabunge wa Yanga, Michael Kadebe

MADAKATARI MGUU NDANI MGUU NJE

  • WATAKIWA KUJIELEZA NDANI YA SIKU SABA
  • WAHADHIRI MUHAS WAWATOLEA UVIVU
 Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya Madaktari waliogoma  katika  hospitali mbalimbali na ametakiwa kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kukiuka maadili ya taaluma.
 Madaktari watakaokumbana na kibano ni wale walio katika  mafunzo kwa vitendo , ambao walifukuzwa katika hospitali za serikali kwa kutakiwa kurudi wizarani,ambapo jana walipewa barua za kutakiwa kujieleza ndani ya siku saba.
 

CHANZO GAZETI LA UHURU LEO

ZIARA YA SHIGELA MKOANI MTWARA

Friday, July 6, 2012
 Katibu Mkuu UVCCM ,Mh.Shigela Martin akihutubia wananchi wa Mtwara
Tambwe Hiza wa CCM Makao Makuu akihutubia wananchi masuala muhimu ya kujenga nchi  na yenye  kuleta maendeleo kwa Taifa
Katibu mkuu wa umoja wa vijana wa CCM Martin Shigela amewataka wananchi wa mkoa wa Mtwara kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao wakati Tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya itakapofika mkoani humo kukusanya maoni ya wananchi,amesema CCM haina agenda yoyote iliyojificha katika upatikanaji wa katiba mpya itakayotokana  na utashi wa wananchi wenyewe ,alitilia mkazo kwa  wananchi kutoa maoni yao kwa amani bila kuingilia uhuru wa wengine,aliwaasa kuangalia mambo ya muhimu ambayo wanaona yatasaidia kuiweka nchi katika amani na kuendelea kutoa fursa ya maendeleo kwa wananchi kama ilivyo sasa,kuhusu mgombea binafsi alisema CCM haipingi kama wapinzani wanavyotangaza na kama wananchi wanalitaka hilo katika kukuza demokrasia nchini waliseme na litatekelezwa bila wasi wasi na kwamba CCM ndiyo itafaidika zaidi kwa kuwa wanachama wake hawataenda upinzani kutafuta nafasi za kugombea kama ilivyo sasa ambapo wanakwenda huko huku wakiamini vyama hivyo havina sera yoyote ya maendeleo  ya Taifa zaidi ya kutaka utawala,alielezea fursa mbali mbali za mkoa huo zilizoletwa na serikali ya CCM na zitakazoendelea kuletwa katika kipindi kifupi kijacho,kabla ya hapo mjumbe aliefuatana naye katika msafara wake Tambwe Hiza alizungumzia hali ya nchi iloivyokwenda mbele kimaendeleo tangu tulipopata uhuru ikiwa nin pamoja na uanzishaji wa shule nyingi za msingi karibu na maeneo wanayoishi wananchi kinyume na hali ilivyokuwa kabla ya kujitawala na miaka ya mwanzo ya uhuru ambapo kila Tarafa ilikuwa na shule moja ya msingi jambo lililopelekea watoto kutembea umbali mkubwa kwenda shule,aliwabeza wanaodai miaka 50 kuwa hakijafanyika kitu kwa kutoa mifano ya ya vyuo vikuu vilivyoanzishwa baada ya uhuru ambavyo havikuwepo kabla idadi ya wanafunzi wanaoingia sekondari hivi sasa akitolea mfano wa idadi ya watoto 5 kati ya watoto 100 waliofaulu waliokuwa wakienda sekondari wakati wa serikali ya awamu ya kwanza kwa kuwa wakoloni hawakujenga za kutosha,wanafunzi waliongezeka kufikia 13 wakati wa awamu ya pili,21 awamu ya tatu na awamu hii ya Rais Kikwete imefikisha 97 kati ya mia huku baadhi ya mikoa ikifikia 100/100

Saturday, July 7, 2012

CCM YAWASHA

Saturday, June 9, 2012

CCM ilipo washa mwanga Jangwani

Waziri wa Ardhi Profesa  Anna Tibaijuka akihutubia
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akihutubia
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akihutubia
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye akihamasisha kwenye mkutano huo, Kushoto ni Mlezi wa mkoa wa Dar, Abdulrahman Kinana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira Uratibu na mahusiano, akizungumza kwenye mkutano huo


Chama Cha Mapinduzi kimedhihirisha wazi ni chama kinachowajibika ipasavyo, Katika Viwanja vya jangwani jana jioni wananchi wa mkoa wa Dar - es salaam walikusanyika kwa wingi kusikia yale muhimu ya chama chao na serikali na wamekubaliana na hayo moja kwa moja.

Wananchi wameelezwa mambo yote ya msingi ikiwa utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya chama,mipango ya kimaendeleo na mafanikio yalofikiwa.